GRM Production

Contact: Email: makupag@gmail.com
Karibu katika Ulimwengu
wa GRM Production

Thursday, December 4, 2014

Neno la Shukrani kutoka kwa Dorka catering na Dorka group of companyInaamiwia vingumu sana kutoa shukrani kwa mtu mmoja mmoja au makundi kutokana na ushirikiano wenu katika kipindi kigumu cha msiba na mazishi ya mpendwa mume wangu na mwenyekiti wa Dorka catering na Dorka group of company 
Marehemu Dr kephas kansolele Ntevi kwaniaba ya familia yangu .Ninapenda kutoa shukrani za dhati  kwa wote walio shiriki kwa njia moja au nyingine kwa kipindi chote cha msiba wa mume wangu.


Kiukweli tulipatwa na kigugumizi ambacho hakisemeki
Ingawa nyote mnastahili kushukuriwa lakini ningependa kutoa shukrani zangu za peke kushukuru madaktari wa Muhimbili na manesi kwenye kitengo cha I.C.U , Dr Kalianyama  mlifanya kazi usiku na mchana kuokoa maisha ya mume wangu lakini mungu alimpenda zaidi, kanisa la Good News Mission Tanzania Pastor kiongozi Jeong na ma pastor na waumini wote hamkuchoka kutuombea na bado mnatuombea tuna shukuru sana, Service Provider wezangu kiukweli mmenionyesha upendo ambao hausemeki, Marafiki zangu na wa familia mlikua na sisi usiku na mchana hamkutuacha, Networks wote waliokua wana shirikiana na mume wangu .Blogs mbalimbali, majirani zetu wa mwenge na Bahari beach , Familia ya Ntevi, Familia ya Wakaombwe na ya Mzee Massau tunapenda kuwashkuru wote kwa upendo na faraja zenu, Sina maneno mazuri ya kuonyesha shukurani zetu za dhati kwa niaba yangu na wanangu, tunaomba mpokee shukurani zetu mwenyezi mungu awaongezee pale mlipo toa.