GRM Production

Contact: Email: makupag@gmail.com
Karibu katika Ulimwengu
wa GRM Production

Thursday, March 31, 2011

Tuesday, March 29, 2011

Masaa 24 na masuper model wangu Sasha na Simon. (24 HRS Family Moments)

Super model wangu Simon akiwa kalala. Nakumbuka ilikuwa mishale ya saa tano usiku (11:00pm) nilipo nyata nakufanikiwa kupata picha hii.  Hii picha nimeipenda sana sijui kama wewe unapicha yako ukiwa umelala. mimi mwenyewe sina!

Hapa ni super model wangu Sasha. na yeye pia nilinyata nikafanikiwa kumpiga picha. Nakumbuka ilikuwa ni mida ya Saa nne na nusu (10:30 Pm). Kweli huyu ni mrembo. 

Swagga la kulala nimelikubali. Safi sana. 

Unajuwa katika mambo ya picha ukikaa muda mrefu huku unaangalia swagga za mamodel kuna muda utapata picha ambayo hauitgemei na kali sana ambayo sio ya kupanga

Kama kichwa cha habari kinavyosema 24 hrs basi nilikuwa na waangalia mamodel tangu wanapoamka mpaka wanapo lala. Sasa na ilipofika wakati wakula nikagundua kuwa  hapo pana kazi yaziada. Kweli wanakula kisharobaro. Nilipouliza kulikoni nikaambia Yoo Bub naogopa kunenema men! Dah

Dah Ulaji huu wa kisharobaro si mchezo.  Ila sijui kwanini wakati wakula watoto wanakuwaga na maswagga. Na huwa mpaka uwatishie ndio wale! wengine wakiona mzazi kaja ndio hali chakula  tena!

Kitu ambacho nimegundua wakati wakula unaweza ukapata picha nzuri za watoto. wanakuwa wapole.

Super model Sasha ndio usipime. Nimegundua yeye na chakula ni paka na panya!

Pole kula basi hata kidogo! Mpaka machozi.

Baada ya kula wakawa tayari kwenda shule.

Kama kawa nikaomba Swagga wakanipa Swagga. Safi sana na hayo ni masaa 24 na super model wetu Simon and Sasha. Nafikiria kuanzisha huduma ya 24 Hrs family moments.

Monday, March 28, 2011

Visura na Kemi Kalikawe. Kweli wabunifu wa mavazi sasahivi wanatisha. Wakoo juu inabidi sasa tuanze kuwaunga mkono kwa kuvaa nguo zao.

Ubunifu wa Kemi katika kisura Final


Wanasema Mganga hajigangi ila kemi umejiganga. Safi sana.  Umejitendea haki wewe mwenyewe.

Nice

Safi 

Mshindi wa kisura 2011


Safi sanaNiceMshindi wa kisura mwaka jana akitowa swagga la mwisho kabla ya kukabizi taji

Nimelikubali hili swagga

Safi