GRM Production

Contact: Email: makupag@gmail.com
Karibu katika Ulimwengu
wa GRM Production

Friday, January 7, 2011

Namshukuru Mungu nimerudi salama kutoka Kuhesabiwa. Nilikwenda Mkowa wa Kilimanjaro Kwa Mapumziko Mafupi. Kwakweli ilikuwa ni likizo ya aina yakeMlima Kilimanjaro

Mlima mrefu kuliko Milima yote Africa

Mji wa moshi ulivyo msafi. Yani kwenye lami unaweza kulia chakula

Kwakweli Mji wa moshi ni zuri sana na pia  msafi sana.

Keep Left cha Arusha. Kiko Moshi
Kipleft cha Saa. Hichi kiko Moshi mjiniHapa ni kwa Deo. kwakweli asubuhi usipo kuja kupata supu hapa lazima utakuwa unamatatizo

Supu ikichemka

Mbuzi akiwa tayari kuhesabiwa

Maunt Meru hotel baada ya kukarabatiwa. Kweli hapa pametulia sana. Nipazuri sana

Hotel Kwa mbele

Mount Meru hotel
Hapa panaitwa Makumba Bay ni Samaki samaki ya moshi ila tofauti na dar hapa waweza pata Mbege au Kitochi. Aksante sana mmiliki wa hapa Kaka Obre kwa kutendea haki mji wa Moshi

Makumba bay kwa ndani. Kwakweli ukija kuhesabiwa na usipo fika hapa basi hesabu inaweza isitimie

Mdau akipata kitochi au mbege akiwa Makumba Bay

Mdau akitowa salamu za mwaka mpa

Mwana sheria wetu akitowa swagga. Pembeni ni mtaalamu wetu wa urembo. Kwakweli huwezi kuhesabiwa bila hata kushika Kata.

Ng'ombe akihesabiwa

Super Model wetu Simon akishuhudia ngombe akihesabiwa


Maharusi watarajiwa wakipakuwa chakula. Machalari. Hichi nichakula kikuu cha wachaga. Pia usipo kula hiki hujahesabiwa.

Mtaalam wetu wa urembo akituma salamu za Mwakampya

Mtaalam wetu waurembo akichat na wadau. Hata Kijijini Naaona face book Inapatikana. Naona Pia alikuwa anachungulia blog ya grm pia ni mpenzi mkubwa wa 8020

Nakumbuka super model wetu Simon kazaliwa tarehe 3 january. Na pia kwakuwa nayeye alikwenda kuhesabiwa basi mtaalam wetu wa urembo akamfanyia suprise party uchagani

Nyanya yake simon nae alishuhudia sherehe ya kuzaliwa ya simon iliyo andaliwa na mtaalam wetu wa urembo

Simon na nyanya yakeNaye sasha alihuzuria Kwenye Sherehe ya kuzaliwa ya super model wetu simon uchagani. 

Simon akikata keki
Hapa ni chagga bites moshi

Mtura ukiwa unaiva. Jamani Mtura ni Soseji za kichaga wanaweka nyama laini ya mbuzi. 

Pia hesabu haiwezi kukamilika bila kula mtura
Kwakweli nitamiss mtura. Huku Dar unaitwa bomu. Ila wanachakachuwa sana hawaweki nyama au steki wanajaza utumbo tuu haswa kitaulo. Mtura hauwekwi kitaulo jamani.
Nakumbuka nilipopita Marangu niliona japo niwaungishe lita 10 za mafuta. Kweli december hii wamefanya biashara

Iko siku jamaa watabadilika na kuweka pump za Uhakika. Uzuri hawachakachui mafuta ila kweli inaitaji moyo kuweka mafuta hapa. Kwa usiyejuwa hichi kituo cha mafuta kiko marangu mtoni na hakuna kituo kingine karibu.