GRM Production

Contact: Email: makupag@gmail.com
Karibu katika Ulimwengu
wa GRM Production

Saturday, January 22, 2011

Ule mchakato wakumsaka kisura bado unaendelea na safari hii tulivamia Monduli. Pia unaweweza kuufwatilia Mchakato huu TBC1 siku ya jumapili saa tatu usiku na Jumatano saa sita mchana.

Vijana waliwasili monduli salama na kuanza kazi ya kumsaka kisura

Kazi haikuwa rahisi ilibidi kukaguwa boma moja baada ya moja

Hapa namuona mmoja ya majaji wa kisura akimwita jaji mwenzake aje ndani maana kuna kisura kamuona

Basi kisura akatolewa na kufanyiwa usaili.

Vijana wakaingia kwenye boma la pili

wakamkuta kisura

Kisuwa akatowa swagga fupi.

Safi

Kuingia kwenye boma la mzee Laiboni tukapata kisura

Kama kawa kisura akatowa swagga baada ya usaili. Na huyu dada anakuja Dar es salaam kwa mara ya kwanza kwaajili yakuanza kambi ya kisura. Naona anafanana na yule super model anaye iwakilisha nchi yetu vizuri 'f. Matata' . Hapa nauwakika mama wa 8020 fashions ukiweka mkono ma anima print ma lotion baada ya mwaka kisura wetu atafika Paris

Ilibidi baba mwenye boma au baba wa familia apewe semina elekezi kuhusu kisura ili akubali binti yake aweze kushiriki. Manake kama sijakosea alizani watu wameleta posa akawa anauliza ng'ombe ziko wapi

Baba mwenye boma akisikiliza kwa umakini


Baba mwenye boma akifanyiwa mahojiano

Kijana wangu hamidu akiwa anachukuwa video huku morani wakiwa makini.

Kwataarifa tuu huyu mzee anawake 35 na watoto 102 wajukuu 15. na ilikujuwa anawatoto wangapi alitupangia mawe chini na tukahesabu. 

Baadhi ya vifaa vya kufanyia ramli

Wakati tunarudi Dar es salaam tulikutana na hii ajali

Poleni sana walio pata hii ajali. Tulipofika tulikuta wameshapelekwa hospitali.