GRM Production

Contact: Email: makupag@gmail.com
Karibu katika Ulimwengu
wa GRM Production

Wednesday, December 22, 2010

Kama nilivyosema mwaka huu GRM Production tunawaletea show ya Kisura. Hichi kipindi kitakuwa kinaruka TBC1 kuanzia mwakani. Ifuatayo ni matayarisho ya kipindi chenyewe Vol 1


Timu yakisura ilipowasili katika jiji la Mwanza. Namuona Mkurugenzi wa Beautiful Tanzane Agency Juliana. Kampuni hii ndio inasimamia na Kumiliki Kisura na Grm Production kazi yetu ni kutengeneza Vipindi vya kisura 2010-2011 Ambavyo hapo january vitaanza kuruka TBC 

Juliana akitoa maelekezo ya awali. Nahisi alikuwa anauliza hao visura wakowapi!

Dada Juliana akifanya mahojiano mafupi ya kufungua kipindi na kuzindua kazi ya kusaka warembo katika jiji la mwanza

Hapa ndipo mchujo ulipofanyika


Visura wakisubiri usaili

Hapa wakifanyiwa usahili. Na haya mashindano huwezi kuchakachuwa. Manake kama wewe haufiki SM 174 urefu na mapaja yakizidizi 92 Sm basi hauwezi kuwa kisura

Kijana wangu Hamidu akichukuwa matukio ya usaili kwa umakini

Hawa ndio majaji

Kisura akifanyiwa usaili

Kisura akionyesha swagga lake 

Hapa kisura akifundishwa namna yakutowa swagga

Kisura akatowa swagga lipya. Hata Flavian Matata katokea kwenyekisura. 

Kisura akitowa swagga

Jaji wetu ambaye ni mshindi wa mwakajana akitowa swagga. Jamani haya mawe yanayo onekana kwa nyuma ni nyara za serikali. Yako kwenye noti ya tsh 1000 pembeni ya picha ya Baba wa taifa.

Ilibidi turekodi baadhi ya clip zakipindi hapa.  

Visura wakipozi  na jaji juu ya mawe!

Kivuko

Kwakweli haya mawe yanavutia sana. ukiambiwa historia yake utasema kweli mbona hayatangazwi. Kuna mzee mmoja jina silikumbuki akikuwa anakatiza katikati ya haya mawe. Akifika Mawe yanasogea! 

Kazi Ikiendelea

Film Director wangu Nago akiwa kazini. Hivi director ukianguka toka huko juu utapona!

Burudani mbalimbali. Nahisi hi ni bongo FLV

Kama mnavyojuwa mmoja wa sponser wa kisura ni HFI na hawa wanaelimisha juu ya HIV. Hapa ilikuwa nisemina fupi kuhusu HIV

Kweli director nakisubiri kipindi kwahamu nije nione hizi shot. unatisha

Presenter akifunga kipindi

Kamera yetu ilinasa watu wakichapana kavukavu. 

Kisura akitowa  Swagga