GRM Production

Contact: Email: makupag@gmail.com
Karibu katika Ulimwengu
wa GRM Production

Tuesday, August 22, 2017

Sanje Waterfall. Maporomoko ya Sanje yako Udzungwa Morogoro.


Nilipotea kidogo nilikuwa kwenye utali wa ndani. Hapa ni Udzungwa ambapo kuna maporomoko ya maji yanaitwa Sanje. 

Sanjewaterfall. Ni poromoko refu Tanzania. Kweli kama unataka utali wa kutembea hii ni sehemu ya kuja. Unafanya zoezi kidogo maana unapanda mlima kwa muda wa kama dakika 45- 1 hrs inategemea na Speed yako- kihenga au kidiamond. Pia Hewa Fresh 
Poromoko No:1 Huku yapo maporomoko Matatu. Hili ndio la kwanza.

Kuna sehemu nzuri sana za kupiga picha Pre wedding, wedding na Etc  niko tayari kurudi tena na Maharusi. 

Simchezo Poromoko no: 2  


Poromoko no 3


Hapa ndio moja ya poromoko linavyoanza. Poromoko no 3. 


Hapa ndio juu kabisa ya hili poromoko No 3 Hapa unaweza fanya picknick Kabisa. Sehemu inafa kutafakari  jinsi ya kujipanga usije ukarudi kijijini. Tatizo ni moja tuu ukipiga yale mavinywaji makali utafurahi sana wakati unakunywa huku unapata bonge la view, ila wakati unarudi chini utajuta maana unatembea kwa muda wa 1 hrs. yani ni kufunga break za migu  hapo ndipo utajua kazi ya vigimbi kwenye mguu lol @@  
Poromoko no 3 aka Sanje kwa chini . 

Huu mti zamani  ulikuwa unatumika kwenye hichi kijiji kama Kengele. ukiugonga unatoa sauti kubwa sababu ndani una nafasi au Pango

Nitawaletea Maswagga zaidi ya Utali wa ndani. Maana hapa pia kuna Nyani -Mbega ambao wanapatina  Uduzungwa tu.