GRM Production

Contact: Email: makupag@gmail.com
Karibu katika Ulimwengu
wa GRM Production

Friday, September 13, 2013

The Wedding of David and Christencious. Onja kidogo jinsi mambo yalivyojiri katika jiji la Moshi.

David and Christencious hakika  walipendeza sana.

Dah nimekubali hili gauni la Christencious. Hakika alilitendea haki.


Nice
Kwa maswagga zaidi zama hapa kwenye read more 
NiceNice


Dah pia nimpongeze Baba na Mama wa David Kwa kutunza gardern. Jamani tangu nasoma shule ya primary walikuwa wanapenda  gardern balaa. Nikipita wakati nakwenda kuogelea Katika shule ya ISM Moshi basi utakuta mzee ananyeshea gardern. Safi sana. Alafu mzee hazeeki kweli sijui siri ya mafanikio yake ila moja ni kumcha Mungu. Namkumbuka sana mzee katika ibada za nyumba kwa nyumba Shanty Town.

Kweli nimekubali rangi ya harusi. Safi sana


Nice


I belive i can fly. Nimewakubali the 'boys'

Swagga

Safi sana. kweli maharusi walifurahi sana 


Hakika Christencious alijipanga sana. Ilipofika jioni alibadili gauni kwa sababu Ndoa nikanisani na ukumbini ni party. Kweli kwa Tanzania bado tunakazi ila mambo yanaanza kubadili. Zile 'protocali' za harusi zinaanza kupungua na watu wanaanza kuweka burudani . Juzi juzi kunaharusi tumefanya mwanzo mpaka mwisho ni Nasaa. Hakuna kucheza hata mziki. Mziki unacheza saa unakwenda kutowa zawadi. Ila harusi hi kweli ilikuwa ni burudani mwanzo mpaka mwisho. Safi sana

The Girls nao walibadili swagga. Safi sanaI love this Pix


Nice. I wish ingekuwa ndio harusi yangu. Safi sana maharusi na kamati. Hakika Jiji la Moshi lilitingishika.
I love this pix

Nice.  Maswagga haya ya barabarani kwa Dar es salaam huwa ningumu. kwanza joto. Maharusi wasipopigwa na kipupwe mchana sijui hizo makeup kama zitabaki, alafu Polisi wetu wa barabarani wakati mwingene hawaoni huruma. Juzi juzi hapa kuna maharusi walipigwa bao kisa wametanua. Upendo kwa Wazazi
The family
Familia ya David ikienda kumchukua mpora. kimila zaidi


David akiwa mpole anamsubiri mpora. Hapa ilikuwa majira ya 7:30 am. Namuona Ndeee. Kijana naona shavu. chezea maisha ya ndoa.

Hatimaye mpora akatoka ndaniKanisa la Lutheran Moshi mjini. Nakumbuka Nilibatizwa  na kupata Kipaimara hapa.
NiceSwagga za gari

Hatimaye moshi tumepata ukumbi wenye Kipupwee. Dah hu ukumbi uko karibia na Kipita shoto cha Arusha

Keki


NdafuuuuuChezea muke wa David


'DonWilliam'. Safi sana. Mzee anajuwa kuimba .
First Dance
Jamani mwisho wakunuku. Wadau wa GRM production nawatakia weekend njema.