GRM Production

Contact: Email: makupag@gmail.com
Karibu katika Ulimwengu
wa GRM Production

Wednesday, August 28, 2013

The Wedding Of Janeth and Derrick. Onja kidogo jinsi mambo yalivyojiri.


Derrick and Janeth hakika walipendeza sana

Nimekubali







Hakika Janeth alilitendea haki gauni lake la harusi

Nice






Kwa Maswagga zaidi zama hapa kwenye Read More

Friday, August 23, 2013

Hellen Ladies Party Coming soon!. Dokoa Kidogo Maandalizi



Hakika Hellen alipendeza sana na Glambox walimtendea haki. 


Hakuna atakayebisha kuwa Hellen Alilitendea haki hili gauni lake. Safi sana. kweli huyu dada alijipanga sana.
Napenda kumpongeza Hellen na Mr wake kwa sababu walijuwa umuhimu wa kumbukumbu katika siku yao muhimu(K Party and Harusi). Tulipiga picha kabla ya kwenda kanisani. Safi sana hi inaonyesha jinsi watu wanavyobadilika na kujuwa kitugani wanakitaka. Mfano  unakuta ndoa inafungwa saa 4pm alafu kanisani watu wanatoka 6pm alafu mtu anataka picha za gardern. hapo hauwezi kupata kumbukumbu nzuri. Na ukimshauri mtu tupige picha kabla ya  kwenda kanisani ;anaona kuwa nikitu ambacho akiwezekani. Eti utamuonaje mchumba kabla ya kufunga ndoa. Mbona wakati wa sendoff walipiga picha???
Kwa kweli kama ukitaka kupiga picha kabla ya kufunga ndoa inabidi uamuwe wewe mwenyewe. Ukiwashirikisha wazazi tuu hapo lazima mambo ya mila yatanza. Huu Ni ushauri tu kwa wale ambao unakuta ndoa inafungwa 4pm.  Mhh ngoja nisionge mengi. ila narudia tena napenda kuwapongeza Hellen na Mr. Kwa Kujipanga. Bado kazi iko jikoni. Ngoja niwaonjeshe picha moja ya harusi

Safi sana. Chakula Bado kiko jikoni







Nimekubali hili swagga. Glam Madam akiona tumetundika viatu anaweza kutukimbiza!!! Natania tuu













Hakika glam madam alikutendea haki












Jamani mwisho wakunuku. Chakula bado kiko jikoni. Wadau wa GRM production  nawatakia weekend njema ila kwetu ndio jumatatu  leo. kesho jumanne.