Kesho tutakuweko kwenye maonyesho ya Harusi Fair pale Diamond Jubilee. Napenda kuwakaribisha kwenye Banda letu. Nitawapa data zaidi baadae |
GRM Production
Contact: Email: makupag@gmail.com
Karibu katika Ulimwengu
wa GRM Production
Thursday, March 31, 2011
Maharusi walio tesa Q1( Jan 2011-March 2011) Grm Production inawatakia maisha mema yenye Upendo na Amani
Tuesday, March 29, 2011
Masaa 24 na masuper model wangu Sasha na Simon. (24 HRS Family Moments)
Hapa ni super model wangu Sasha. na yeye pia nilinyata nikafanikiwa kumpiga picha. Nakumbuka ilikuwa ni mida ya Saa nne na nusu (10:30 Pm). Kweli huyu ni mrembo. |
Swagga la kulala nimelikubali. Safi sana. |
Unajuwa katika mambo ya picha ukikaa muda mrefu huku unaangalia swagga za mamodel kuna muda utapata picha ambayo hauitgemei na kali sana ambayo sio ya kupanga |
Dah Ulaji huu wa kisharobaro si mchezo. Ila sijui kwanini wakati wakula watoto wanakuwaga na maswagga. Na huwa mpaka uwatishie ndio wale! wengine wakiona mzazi kaja ndio hali chakula tena! |
Kitu ambacho nimegundua wakati wakula unaweza ukapata picha nzuri za watoto. wanakuwa wapole. |
Super model Sasha ndio usipime. Nimegundua yeye na chakula ni paka na panya! |
Pole kula basi hata kidogo! Mpaka machozi. |
Baada ya kula wakawa tayari kwenda shule. |
Kama kawa nikaomba Swagga wakanipa Swagga. Safi sana na hayo ni masaa 24 na super model wetu Simon and Sasha. Nafikiria kuanzisha huduma ya 24 Hrs family moments. |
Monday, March 28, 2011
Visura na Kemi Kalikawe. Kweli wabunifu wa mavazi sasahivi wanatisha. Wakoo juu inabidi sasa tuanze kuwaunga mkono kwa kuvaa nguo zao.
Subscribe to:
Posts (Atom)